SW | EN
KARIBU HAI RURAL TEACHERS SACCOS LTD

SACCOS Bora inayothamini Wanachama wake.

Tunakuunga mkono katika kila hatua unayochukua. Tumejizatiti kuwawezesha wanachama wetu kwa ukuaji wa Uchumi wao.

Tsh 21.8 B+ Thamani ya Rasilimali Tunazomiliki
97% Kuridhika kwa Wanachama
26+ Miaka ya Huduma
Tsh 21.8 B+ Thamani ya Rasilimali Tunazomiliki
97% Kuridhika kwa Wanachama
26+ Miaka ya Huduma
Usalama wa Kifedha Imesajiliwa na TCDC Wanachama 3,200+ Faragha ya Mwanachama Huduma Bora za Kifedha Wilaya ya Hai, Kilimanjaro Usalama wa Kifedha Imesajiliwa na TCDC Wanachama 3,200+ Faragha ya Mwanachama Mikopo ya haraka na nafuu Tumesajiliwa PDPC

Bidhaa Zetu

Katika HRT SACCOS LTD, tumejizatiti kubadilisha maisha ya wanachama wetu kupitia huduma za kifedha zinazoaminika na kuendeshwa na wanachama wenyewe.

Hisa za Msingi na Hiari

Mwanachama atanunua Hisa za msingi zisizopungua 70 sawa na TZS 700,000 (Thamani ya Hisa moja ni TZS 10,000) ili kumuwezesha kuwa mmiliki wa Chama. Pia anaruhusiwa kununua Hisa za hiari (zaidi ya TZS 700,000) ilimradi asizidi 20% ya Hisa zote za Chama.

Soma zaidi

Huduma za Amana (Fixed & Amana Toto)

Kuweka na kutoa fedha kwa usalama wakati wowote. Inajumuisha Amana ya Muda Maalum (Fixed Deposit) yenye faida ya riba 7-9% kwa mwaka, na Amana Toto kuanzia TZS 10,000 kila mwezi kwa ajili ya maandalizi ya mtoto chini ya miaka 18.

Soma zaidi

Akiba na Akiba ya Dharura

Kuweka akiba kuanzia TZS 25,000 kila mwezi inayopata faida ya 7-9% kwa mwaka na kumpa mwanachama fursa ya kukopeshwa mara 4 ya Akiba zake. Pia kuna Akiba ya Dharura (mpaka TZS 600,000) inayowezesha kukopeshwa mara 5 ya akiba hiyo.

Soma zaidi

Mikopo ya Maendeleo

Mkopo kwa ajili ya elimu, biashara, kilimo na ufugaji, ujenzi, ununuzi wa vyombo vya usafiri, viwanja na shughuli zote za maendeleo. Kiwango cha juu ni TZS 40,000,000 na muda wa marejesho ni mwezi 1 mpaka miezi 60 kwa riba nafuu sana.

Soma zaidi

Mikopo ya Dharura

Mkopo wa haraka kwa ajili ya majanga kama vile kuugua, kufiwa, kuibiwa au maafa kuanzia TZS 50,000 mpaka TZS 3,000,000. Muda wa marejesho ni miezi 1 hadi 24 kwa riba nafuu sana. Unapatikana siku hiyo hiyo ya ombi.

Soma zaidi

Mikopo ya Safina (Top-Up)

Inamruhusu Mwanachama mwenye mkopo unaoendelea kulipwa kukopa mkopo mkubwa zaidi (Top up) na kulipa deni lote analodaiwa kutoka katika mkopo huo mpya. Vigezo na marejesho ni sawa na Mkopo wa Maendeleo kwa riba nafuu sana.

Soma zaidi

Stress Free (Salary Advance)

Mkopo wa mshahara wa haraka wa kiwango cha juu cha TZS 300,000 mwenye muda wa marejesho wa mwezi mmoja (1) kwa riba nafuu sana. Mkopo huu unapatikana siku ile ile aliyoomba Mwanachama.

Soma zaidi
26+ Miaka ya Uzoefu

HAI RURAL TEACHERS SACCOS LTD

HRT SACCOS LTD, tunaamini katika nguvu ya umoja na maendeleo ya Kiuchumi. Iwe wewe tayari uko pamoja nasi au unapanga kujiunga, kesho yako huanza hapa na tutakwenda nawe hatua kwa hatua.

Dhamira Yetu

Kutoa huduma zinazodumu, zinazopatikana kwa urahisi, na zenye kuwajali Wanachama.

Maono Yetu

Kuwa SACCOS inayoongoza nchini Tanzania, inayojulikana kwa ubora wa Huduma na uaminifu.

Lengo Letu

Kuimarisha hali ya kiuchumi ya wanachama kwa kukuza utamaduni wa kuweka akiba na kukopesha kwa tija.

Kuhusu Sisi

Je, uko tayari Kukuza Uchumi Wako?

Jiunge na HRT Saccos leo na ufurahie huduma bora za kifedha kwa maendeleo yako.

Timu Yetu

Watoa huduma wetu waliojitolea kutoa huduma bora kwa wanachama wetu.

Mwl. ALEX WARIOBA - Mwenyekiti wa Bodi
Mwl. ALEX WARIOBA
Mwenyekiti wa Bodi
MS. UPENDO LYATUU - MENEJA MKUU
MS. UPENDO LYATUU
MENEJA MKUU
Godgift E. Gadiel - MHASIBU MKUU
Godgift E. Gadiel
MHASIBU MKUU
EMANUEL  BURA - ICT Officer | Application Programmer
EMANUEL BURA
ICT Officer | Application Programmer

Habari za Hivi Punde

Pata taarifa mbalimbali kuhusu chama chetu, elimu ya ushirika, na habari za uchumi.

Kuu
Habari
Mkutano mkuu wa Kwanza wa Dondoo kwa Wanachama 2026

Mkutano wa Dondoo 2026 ulifanyika Filomena, Bomang’ombe, ukiwakutanisha wanachama wa Tarafa ya Masam...

07 Sep, 2026 Soma Zaidi

Wanachama Wetu Wanasemaje?

Pata Taarifa kwa Barua Pepe

Jiunge na jarida letu kupata habari za hivi punde moja kwa moja kwenye barua pepe yako.

×

Uhahiki wa Mwanachama

Tafadhali weka Check Number yako ili kuendelea.

×

Vigezo vya Kujiunga

Tafadhali weka taarifa zako za mshahara ili kuona kama una vigezo vya kujiunga na SACCOS.

Wasiliana Nasi
Mwenyekiti Online
Meneja Online
Afisa TEHAMA Online
Mhasibu Online
Afisa Mikopo Online