Sisi ni Chama cha Akiba na Mikopo kinachojitoa kuinua hali ya kiuchumi ya wanachama wetu kupitia huduma bora za kifedha.
Ilianzishwa tukiwa na lengo moja: kutoa huduma bora za kifedha zinazopatikana kwa urahisi na zenye riba nafuu. Leo, tuko imara na tunaendelea kukua pamoja na wanachama wetu.
Kutoa huduma zinazodumu, zinazopatikana kwa urahisi, na zenye kuwajali Wanachama.
Kuwa SACCOS inayoongoza nchini Tanzania, inayojulikana kwa ubora wa Huduma na uaminifu.
Kuimarisha hali ya kiuchumi ya wanachama kwa kukuza utamaduni wa kuweka akiba na kukopesha kwa tija.
Hatua muhimu tulizopitia tangu kuanzishwa kwetu hadi leo.
Hai Rural Teachers SACCOS ilianzishwa na Wanachama waanzilishi 67 waliounganishwa na dira ya pamoja ya kuwawezesha walimu Kiuchumi.
Hai Rural Teachers SACCOS imepata ukuaji wa haraka kupitia ongezeko la wanachama na huduma bora za kifedha.
Kutumia suluhisho za mifumo ya kibenki katika uendeshaji wa shughuli za kila siku
Tulifikia Wanachama 2,000 na kupanua wigo wa huduma na bidhaa zetu kujumuisha uwekezaji na mipango ya Kimkakati.
Miongoni mwa SACCOS zinazofanya vyema Kilimanjaro na Tanzania kwa ujumla
Timu yenye uzoefu waliojitolea kutoa huduma bora na kuleta maendeleo kwa Wanachama wetu.
Wanachama Waliojiunga
Mikopo Iliyotolewa
Hisa za Wanachama
Uzoefu wa Miaka
Tuzo za Ushirika