SW | EN

Tuna Majibu ya Maswali Yako

Maswali Yanayoulizwa Sana

Hupati unachotafuta? Wasiliana nasi na tutakujibu ndani ya masaa 24.

Nani anastahili kujiunga na HRT SACCOS LTD?
Wanaostahili kujiunga ni pamoja na:
1. Wafanyakazi wa serikali kuu na serikali za mitaa wa wilaya za Hai na Siha.
2. Wastaafu wa Wilaya za Hai na Siha wakiwa Wanachama.
3. Wenza wa ndoa wa Wanachama wa Hai Rural Teachers SACCOS.
4. Watumishi katika Wilaya za Hai na Siha waliohamia Wilaya na Taasisi nyingine za Serikali.
Ni vigezo gani na gharama za kujiunga na Chama?
Vigezo na mahitaji ya kujiunga ni:
1. Ada ya kiingilio: TZS 30,000.
2. Hati ya mshahara (Salary slip) ya mwezi wa karibuni.
3. Picha 2 za rangi za pasipoti (Passport size).
Thamani ya hisa na kiwango cha chini cha hisa za msingi ni ngapi?
Thamani ya hisa moja ni TZS 10,000. Mwanachama anapaswa kununua hisa za msingi zisizopungua 70 sawa na TZS 700,000 ili kuwa mmiliki kamili wa Chama. Pia anaruhusiwa kununua hisa za hiari zisizozidi 20% ya hisa zote za Chama.
Je, kuna aina gani za akiba na nawezaje kukopa kupitia akiba yangu?
1. Akiba ya Kawaida: Kuanzia TZS 25,000 kila mwezi. Hutumika kama dhamana ya mkopo ambapo mwanachama hukopeshwa mara 4 ya akiba yake, na kupata faida ya riba 7% hadi 9% kwa mwaka.
2. Akiba ya Dharura: Kiwango cha juu TZS 600,000. Hutumika kama dhamana ya mkopo wa dharura na mwanachama hukopeshwa mara 5 ya akiba ya dharura.
Je, HRT SACCOS inatoa aina gani za mikopo na viwango vya riba ni vipi?
HRT SACCOS LTD inatoa aina 4 za mikopo:
1. Mkopo wa Maendeleo: Hadi TZS 40,000,000, marejesho miezi 1 - 60, riba 15% kwa mwaka kwa salio linalopungua.
2. Mkopo wa Dharura: TZS 50,000 hadi TZS 3,000,000, marejesho miezi 1 - 24, riba 13% kwa mwaka kwa salio linalopungua (hutolewa siku ile ile ya maombi).
3. Mkopo wa Safina (Top-Up): Kukopa zaidi na kulipa salio la deni la zamani.
4. Stress Free (Salary Advance): Hadi TZS 300,000, marejesho mwezi 1, riba 3% kwa mwezi mmoja tu.
Je, kuna gharama zozote za maombi ya mkopo (Application Fees)?
Hapana. Hakuna gharama yoyote ya fomu au maombi ya mkopo (Loan application fee ni TZS 0).
Je, Mfuko wa Kinga ya Majanga ya Mikopo hufanyaje kazi?
Mikopo kuanzia TZS 1,500,001 hukatwa 1% kama kinga ya majanga na kuingizwa kwenye Mfuko wa Majanga wa Chama unaotoa:
1. Mwanachama akifariki: Mkopo wote uliosalia unalipwa na mfuko.
2. Pole ya msiba wa mwanachama: Familia hupewa TZS 400,000.
3. Pole ya msiba wa mwenza wa ndoa: Mwanachama hupewa TZS 300,000.
4. Pole ya msiba wa mtoto wa kumzaa (chini ya miaka 21): Mwanachama hupewa TZS 300,000.
Kuna huduma gani za Amana na uwekezaji?
1. Amana ya Kawaida: Kuweka na kutoa fedha wakati wowote bila vikwazo.
2. Amana ya Muda Maalum (Fixed Deposit): Kuwekeza kwa muda maalum na kupata faida ya riba 7% hadi 9% kwa mwaka.
3. Amana Toto: Huendeshwa na mzazi kuanzia TZS 10,000/mwezi hadi mtoto afikishe miaka 18 (kutoa fedha inaruhusiwa mara 2 kwa mwaka hadi 80% ya bakaa).
Ofisi za HRT SACCOS zipo wapi na muda wa kazi ni upi?
Makao Makuu: Bomang'ombe, Wilaya ya Hai, Kilimanjaro (Karibu na Ofisi za Ardhi, Ujenzi au TAKUKURU), S.L.P 8 Hai.
Tawi Dogo: Wilaya ya Siha, Kanisa la KKKT Sanya Juu.
Simu: 0272750208 / 0754928023 / 0715371153.
Muda wa Kazi: Jumatatu - Ijumaa (Saa 2:00 Asubuhi - 9:30 Alasiri), Jumamosi (Saa 2:00 Asubuhi - 6:30 Adhuhuri).
Je, utaratibu wa kusitisha uanachama upoje?
Mwanachama anayetaka kusitisha uanachama anatoa taarifa rasmi kwa maandishi, na stahiki zake zote za akiba na hisa zitalipwa baada ya siku 90 kwa mujibu wa sheria za Ushirika.

Je, uko tayari Kukuza Uchumi Wako?

Jiunge na HRT Saccos leo na ufurahie huduma bora za kifedha kwa maendeleo yako.

×

Uhahiki wa Mwanachama

Tafadhali weka Check Number yako ili kuendelea.

×

Vigezo vya Kujiunga

Tafadhali weka taarifa zako za mshahara ili kuona kama una vigezo vya kujiunga na SACCOS.

Wasiliana Nasi
Mwenyekiti Online
Meneja Online
Afisa TEHAMA Online
Mhasibu Online
Afisa Mikopo Online