SW | EN

Bidhaa na Huduma Zetu

Suluhisho kwa Kila Lengo la Kifedha

Iwe unaanza sasa au unatafuta kukuza utajiri wako, tuna suluhisho lililoundwa kwa ajili yako.

Hisa za Msingi na Hiari

Mwanachama atanunua Hisa za msingi zisizopungua 70 sawa na TZS 700,000 (Thamani ya Hisa moja ni TZS 10,000) ili kumuwezesha kuwa mmiliki wa Chama. Pia anaruhusiwa kununua Hisa za hiari (zaidi ya TZS 700,000) ilimradi asizidi 20% ya Hisa zote za Chama.

Uliza zaidi

Huduma za Amana (Fixed & Amana Toto)

Kuweka na kutoa fedha kwa usalama wakati wowote. Inajumuisha Amana ya Muda Maalum (Fixed Deposit) yenye faida ya riba 7-9% kwa mwaka, na Amana Toto kuanzia TZS 10,000 kila mwezi kwa ajili ya maandalizi ya mtoto chini ya miaka 18.

Uliza zaidi

Akiba na Akiba ya Dharura

Kuweka akiba kuanzia TZS 25,000 kila mwezi inayopata faida ya 7-9% kwa mwaka na kumpa mwanachama fursa ya kukopeshwa mara 4 ya Akiba zake. Pia kuna Akiba ya Dharura (mpaka TZS 600,000) inayowezesha kukopeshwa mara 5 ya akiba hiyo.

Uliza zaidi

Mikopo ya Maendeleo

Mkopo kwa ajili ya elimu, biashara, kilimo na ufugaji, ujenzi, ununuzi wa vyombo vya usafiri, viwanja na shughuli zote za maendeleo. Kiwango cha juu ni TZS 40,000,000 na muda wa marejesho ni mwezi 1 mpaka miezi 60 kwa riba nafuu sana.

Uliza zaidi

Mikopo ya Dharura

Mkopo wa haraka kwa ajili ya majanga kama vile kuugua, kufiwa, kuibiwa au maafa kuanzia TZS 50,000 mpaka TZS 3,000,000. Muda wa marejesho ni miezi 1 hadi 24 kwa riba nafuu sana. Unapatikana siku hiyo hiyo ya ombi.

Uliza zaidi

Mikopo ya Safina (Top-Up)

Inamruhusu Mwanachama mwenye mkopo unaoendelea kulipwa kukopa mkopo mkubwa zaidi (Top up) na kulipa deni lote analodaiwa kutoka katika mkopo huo mpya. Vigezo na marejesho ni sawa na Mkopo wa Maendeleo kwa riba nafuu sana.

Uliza zaidi

Stress Free (Salary Advance)

Mkopo wa mshahara wa haraka wa kiwango cha juu cha TZS 300,000 mwenye muda wa marejesho wa mwezi mmoja (1) kwa riba nafuu sana. Mkopo huu unapatikana siku ile ile aliyoomba Mwanachama.

Uliza zaidi

Kuanza ni Rahisi

01
Wasiliana Nasi

Wasiliana na ofisi zetu kwa maelekezo zaidi na ushauri kuhusu huduma unayohitaji.

02
Tathmini ya Mahitaji

Tunatathmini mahitaji yako na kukuongoza kuchagua huduma bora inayoendana na malengo yako.

03
Utoaji wa Huduma

Tunashughulikia ombi lako kwa haraka na kukupatia huduma uliyochagua kwa ufanisi mkubwa.

04
Usaidizi Endelevu

Tunaendelea kuwa nawe kutoa mwongozo ili kuhakikisha unanufaika kikamilifu na huduma zetu.

Ufumbuzi wa Kifedha unaokujali

Tunatoa huduma mbalimbali zilizoundwa kumpa mwanachama uhuru wa kifedha, kuanzia umiliki kupitia hisa, kukuza akiba, hadi uwekezaji wenye faida kubwa kwa ajili ya mustakabali wako na familia yako.

Hisa za Umiliki

Hisa zinakufanya kuwa mmiliki halali wa SACCOS. Utapata gawio la faida (Dividends) kila mwaka kulingana na kiasi cha hisa ulizowekeza, huku ukishiriki katika maamuzi makuu ya chama.

Akiba Endelevu

Hiki ni kigezo kikuu cha kuwa mwanachama. Akiba yako ndiyo msingi wa kukuza mtaji wa chama na inakupa sifa ya kupata mikopo nafuu inayozidi hadi mara tatu ya akiba uliyonayo.

Mikopo Nafuu & Haraka

Pata mikopo yenye riba ndogo kuanzia ya dharura hadi ya maendeleo. Tunashughulikia maombi yako kwa weledi na kasi ili kutimiza mahitaji yako ya kifedha kwa wakati.

Amana za Kawaida

Weka na utoe fedha zako wakati wowote bila gharama yoyote ya makato wala ada za mwezi. Hii ni njia salama na rahisi ya kutunza fedha zako kwa matumizi ya kila siku.

Amana ya Muda (Fixed)

Wekeza fedha zako kwa muda maalum (miezi 3, 6 au 12) na upate faida kubwa ya kuanzia 7% hadi 9% kwa mwaka. Njia bora ya kukuza fedha zako kwa usalama bila riski.

Amana ya Toto

Andaa mustakabali mzuri wa watoto wako. Hii ni akiba maalum kwa ajili ya elimu au malengo mengine ya baadaye ya watoto wako kwa misingi imara ya kifedha.

Je, unahitaji Mkopo au Kukuza Uchumi Wako?

Omba mkopo wa maendeleo, dharura au salary advance kwa urahisi na haraka mtandaoni, au jiunge na HRT Saccos leo.

×

Uhahiki wa Mwanachama

Tafadhali weka Check Number yako ili kuendelea.

×

Vigezo vya Kujiunga

Tafadhali weka taarifa zako za mshahara ili kuona kama una vigezo vya kujiunga na SACCOS.

Wasiliana Nasi
Mwenyekiti Online
Meneja Online
Afisa TEHAMA Online
Mhasibu Online
Afisa Mikopo Online